Kwanini Binti wa Yesu Blog?

Hello binti wa Yesu, hope uko poa na mambo yanaenda upande wako. Leo nimekuletea makala nyingine nzuri yenye lengo la kukujuza kwanini blog hii itakufaa wewe kama binti uliyeokoka tena mseja (single). Niko hapa kukupa sababu za wewe kubaki nami na kuwa msomaji (na kuchangia) wangu wa kudumu.

1. Binti wa Yesu ni Chombo cha Bwana.

Blog hii haijaanzishwa kwa sababu zangu binafsi ili kujifurahisha (hobby). Imeanzishwa ili kutii kile nilichoambiwa na Mungu nifanye therefore ni chombo kamili kwaajili ya kusudi la kumtumikia Mungu kupitia uandishi. Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kwamba ipo siku nitakuwa blogger, na si hilo tu, sikuwahi kufikiri kwamba Mungu anaweza kutumia blogging kama namna ya kumtumikia. Lakini I guess kwa Mungu yote yanawezekana na kupitia hili nimejifunza kutomuweka Mungu ndani ya box kwa habari ya utendaji Wake.

2. Binti wa Yesu Inasimamia Ukweli.

Nikisema ukweli namaanisha mimi kama mwandishi wa blog hii siko hapa kuigiza/ kuonekana naweza sana au bora kuliko wengine. I will be as authentic and vulnerable as I can sawasawa na mapenzi Yake. Lengo ni kuonyesha namna ambavyo sisi wenyewe hatuwezi na hivyo tunamhitaji Kristo vilivyo ili kumpendeza Mungu. Lakini pia kukusaidia wewe binti mwenzangu kutambua kuwa hauko peke yako katika yale unyayoyapitia katika ubinti wako, kwani unachokumbana nacho wewe ndicho ninachokumbana nacho pia (1 Petro 5:9).

3. Binti wa Yesu Inagusa Maeneo Muhimu Kwako Kama Binti.

Blog hii inagusa maeneo matatu makuu nayo ni;
i. Useja (Singleness)
ii. Kusudi la Kuwepo (Purpose for Existence)
iii. Kusubiri kwa Usafi (Celibacy & Purity).

Nikianza na useja, Binti wa Yesu ipo kwaajili ya kukupa kwanza taarifa sahihi maana kuna taarifa nyingi zisizo sahihi zilizosambazwa na zinazoendelea kusambazwa na mwovu shetani kwa habari ya nini maana halisi ya useja, umuhimu wake, nini kifanyike wakati wa useja na namna unavyoweza kuufurahia wakati huu pasipo kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

Kwa habari ya kusudi, Binti wa Yesu itakusaidia kutambua kusudi la kuzaliwa kwako na mchakato mzima wa kutembea katika kusudi hilo kikamilifu.

Eneo la tatu likiwa ni celibacy yaani kuamua kusubiri kushiriki tendo la ndoa ili kumtii Mungu na kutimiza mapenzi Yake. Neno la Mungu liko wazi juu ya wakati/mazingira sahihi ya kushiriki tendo la ndoa na ni katika ndoa pekee na si kinyume na hapo (1 Thesal. 4:3). Hivyo basi, Binti wa Yesu ipo kwaajili ya kukutia moyo, kukuwezesha kukupa maarifa na hatimaye uweze kusubiri katika usafi kwa mafanikio mpaka ndoa.

Nafikiri sababu hizi zinatosha kabisa kukufanya ubaki nami katika Binti wa Yesu Blog. Nakupenda💝.

Advertisements

Karibu Binti wa Yesu 😘

Ahsante kwa kuungana nami!

Mambo, naitwa Upendo Masenga, mwandishi wa blog hii. Blog hii nimeianzisha kwa lengo la kuifanya jukwaa la kuweza kuwaleta pamoja mabinti waliookoka na walio katika useja (singleness). Lengo likiwa ni;

1. Kuwahamasisha mabinti hao waseja kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

2. Kutiana moyo wakati wa kusubiri kwa usafi (celibacy & purity).

3. Kuwawezesha kupitia taarifa sahihi na nyenzo mbalimbali kuelewa kusudi la kuumbwa kwao kama mtu binafsi (individual).

Karibu tusafiri pamoja katika safari hii ya useja (singleness).